sPORTS nEWS: Chiji wa Simba na Yanga atimukia Coastal Union...#share

TIMU ya soka ya Coasta Union ya Jijini Tanga, itaanza mazoezi kesho (Jumanne) kwenye uwanja wa Mkwakwani kujiwinda na Ligi Daraja la Kwanza (FDL), inayotarajiwa kuanza mwezi ujao huku ikitangaza nyota wake wapya iliyowasajili msimu huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu hiyo Ahmed Hilal ‘Aurora’, amesema kazi ya usajili haina rahisi kutokana na kwamba kabla hawakuwa na fedha hivyo baada ya kurudisha umoja wameweza kusajili wachezaji wadhoefu watakaowasaidia kupanda daraja msimu huu.

Aurora amewataja baadhi ya wachezaji wapya kuwa ni pamoja na mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Simba na Yanga Athumani Idd ‘Chuji’, Hussein Sharrif ‘Cassilas’, Salvatory Ntebe kutoka Ndanda FC, Ramadhani Hassain kutoka Mbeya City, Maulid Rajab ‘Mau’ African Sports, Hilal Juma Mtibwa, Ramadhani Mussa Pamba, Ibrahim Ndanda, Baraka Jafar na Omary Salum kutoka African Lyion.

Aurora ametaja wachezaji wengine ni pamoja na mfungaji bora wa Ndondo Cup iliyomalizika hivi karibuni Jijini Dar es salaam Rashid Roshi, Exavery Emanuel, Rahim Aziz Afrikan Lyon, Sagaf  Kabaki, Bakari Mtwiku, Bakari Nondo, Said Jeilani na Abubakari Kinanda ‘Mapara’ kutoka malindi ya Zanzibar.

Mwenyekiti huyo amesema usajili waliofanya ulizingatia mahitaji yaliyopo pamoja na tathimini waliyofanya baada ya kushuka daraja na kisha mwaka jana kushindwa kurejea Ligi kuu lakini pia umefanyika baada ya kuzika makundi yao na mpasuko.

Katibu wa klabu hiyo Nassor Kibabedi amesema mazoezi yataanza kesho kwenye uwanja wa Mkwakwani asubuhi kishajioni yatafanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Galanos ambako mwalimu atakuwa Joseph Lazaro


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search