nEWS: Vijiji vitatu Kishapu kunufaika na mradi wa visima vya maji.. #share
Diwani wa Kata ya Mwaweja, Makanasa Kishiwa akifungua pazia kuweka jiwe la msingi ujenzi wa moja ya visima saba vilivyojengwa, hafla iliyofanyika kijiji cha Mwajiginya kata ya Mwaweja.
Diwani wa Kata ya Mwaweja, Makanasa Kishiwa akizungumza na wananchi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi.
Mhandisi wa Maji Wilaya ya Kishapu, Lucas Said akizungumza na wananchi katika hafla hiyo.
Mhandisi wa Maji wilaya ya Kishapu, Lucas Said akitoa maelezo kuhusu namna nyenzo ya kunawia mikono kwa mtu aliyetoa kujisadia inavyofanya kazi na kumuepusha na maradhi.
Diwani wa Kata ya Mwaweja, Makanasa Kishiwa akinawa maji safi wakati alipooneshwa nyenzo maalumu kwa ajili ya kunawa mikono.
Mratibu wa TCRS Kishapu, Oscar Lutenge akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Ofisa Kilimo kata ya Ngofila, Genes Tarimo akitoa maelezo kuhusu teknolojia rahisi ya kuchemsha maji bila kutumia nishati ya kuni au mkaa ambayo husaidia kuhifadhi mazingira.
Kikundi cha kwaya kutoka kata ya Mwaweja kikitoa burudani iliyoambatana na ujumbe wa kuhifadhi mazingira.
Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
Mafundi wakiwa katika hatua ya mwisho ya ujenzi wa mojawapo ya visima hivyo.
Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo.
Wananchi wa vijiji vya Mwajiginya A, Ubata na Mwaweja wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wanatarajia kunufaika na mradi wa visima vya maji saba mwaka huu.
Hii ni baada ya kuwekwa jiwe la msingi ujenzi wa visima hivyo vyenye thamani ya sh. milioni 61.9 uliofadhiliwa na Shirika la Norwegian Church Aid-Tanzania (NCA) likishirikiana na TCRS pamoja na halmashauri ya Kishapu huku sh. milioni 1.6 zikiwa ni ndugu za wananchi.
Amezindua mradi huo, Diwani wa Kata ya Mwaweja, Makanasa Kishiwa alishukuru mashirika hayo kwa kuchangia shughuli za maendeleo na kuwataka wananchi waibue miradi ya maendeleo ili Serikali iwachangie.
Amesema wananchi wana jukumu la kuibua na kuanzisha miradi ili na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo iwaunge mkono kwa kutekeleza miradi hiyo.
“Ninyi wananchi muibue miradi na Serikali itapeleka fedha kuikamilisha, haiwezi kutoa fedha kwa sehemu ambayo haina mradi hivyo nawaomba mchangamkie fursa hiyo,” amesema diwani.
Kishiwa ameongeza kwa kusisitiza kuwa sheria ziwabane wananchi wasiokuwa waaminifu wanaotumia muda wao kufanya uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali.
Ofisa miradi wa NCA, Zachayo Makobero alisema visima hivyo vitahudumia wananchi 2100 watakaopata maji ndani ya mita 400 kama sera ya maji inavyosema huku 9200 watapata huduma hiyo nje ya umbali wa mita hizo.
Amesema elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na usafi wa mazingira kwa kata hiyo na zingine wilayani humo na vijiji vyake imeendela kutolewa ikiwa ni mwendelezo wa kampeni zilizofanyika mwaka jana.
Kwa upande wake, Mhandisi wa maji wilaya ya Kishapu, Lucas Said amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji na kupanda miti ili kuepuka visikauke na kusababisha ukame.
Pia, amewataka kutunza miundombinu ya maji kwani imejengwa kwa gharama kubwa ili kuwahudumia huku akiizitaka kamati za maji vijijini kufanya kazi yake ipasavyo katika kuhudumia wananchi.
Mhandisi Said ameipongeza TCRS kwa kazi nzuri ya kuelimisha na kuhamasisha wananchi utunzaji mazingira na kuwataka wajenge na kutumia vyoo ili kuepuka maradhi.

Na: Robert Hokororo
No comments:
Post a Comment