nEWS: Waziri Mwigulu ataka gereza kuu Iringa lijengwe haraka.. #share

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa MWIGULU NCHEMBA ameuagiza uongozi wa Jeshi la Magereza Mkoani Iringa kuanza mara moja utekelezaji wa mpango wa kuhamisha gereza kuu la mkoa huo kwa kuanza ujenzi wa gereza jipya katika eneo la Mlolo.



Kuhama kwa gereza hilo lililopo katikati ya Mji wa Iringa kunatokana na kubanana kati ya gereza na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.


Muda mfupi baada ya kuteuliwa, Waziri MWIGULU alipotembelea gereza hilo la mkoa alikubali ombi la uongozi wa Mkoa wa Iringa kuhamisha gereza ili kupisha upanuzi wa hospitali hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, Bw. AFWILILE MWAKIJUNGU amesema mwingiliano uliopo katika eneo lilipo Gereza Kuu la Iringa kwa sasa siyo rafiki na kwamba eneo hilo la Mlolo litaongeza ufanisi kwa Magereza Iringa kutokana na uwepo wa eneo kubwa ambalo linaweza kutumika kwa uzalishaji mali kupitia kilimo na ufugaji.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search