RELIEVED: Kumhusu Madam Sepetu,.. Tundu Lissu 'kaichomolea' Mahakama kuhusu kutumia 'bahasha yenye msokoto wa bhangi'.. #share

Wakili Msomi aliesimama kumtetea mwanadada Superstar kwenye tasnia ya 'ulimbwende & filamu' nchini mrembo Wema Sepetu, Tundu Lissu amekinukisha Mahakamani baada ya kukataa kata-kata  kupokelewa kwa kielelezo cha bahasha yenye ushahidi wa msokoto mmoja na vipisi 2 vya bangi Mahakamani, vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema Sepetu.




Lissu amepinga kielelezo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kumuongoza shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima.

Aidha, Lissu amedai kuwa kielelezo cha ushahidi kisipokelewe kwa sababu ndani ya bahasha yenye ushahidi kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi akisema vipisi 2 vya bhangi havijitoshelezi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search