sPORTS nEWS: Baada ya Manchester United kupokea kichapo toka kwa Real Madrid, Matic ampa Tano Lukaku..#share
Licha ya Klabu ya Manchester United
kufungwa jana, Nemanja Matic anauhakika kuwa mchezaji mwenzake Romelu Lukaku atakuwa
mtambo wa kufunga magoli katika msimu ujao.
Mashetani Wekundu jana usiku walipoteza mbele ya Klabu ya
Real Madrid kwa kipigo cha goli 2-1 kwa magoli ya Casemiro na Isco kabla ya Lukaku
kuirudisha mcezoni timu yake ya Manchester United baada ya kufunga goli dakika
ya 62 ya mchezo.
Mshambuliaji huyo namba tisa alifunga goli la kwanza la
mashindano ndani ya kikosi chake cha United United katika mchezo wenye
ushindani ambapo alifunga kwa kupiga shuti baada ya shuti kali la Matic kutemwa
mbele yake na Goli kipa wa Real Madirid Keylor Navas.
Kabla ya kufunga goli hilo Lukaku alikosa nafasi ya wazi, lakini
baada ya mchezo huo Matic alikuwa na Imani kwamba goli la Mbeligiji ndiyo mwanzo wa magoli mengine.
“Ni jambo la muhimu
sana kwetu kwa mshambuliaji wetu kufunga magoli,” Matic ameiambia “Ni muhimu
sana kwa kujiamini.
“Kama unavyojua alikosa nafasi nzuri, lakini hilo linaweza kutokea, ni mpira. Lakini
ninafuraha kwa kwa yeye kufunga baada ya kukosa nafasi ya kwanza na ni kwamba
atafunga magoli mengi msimu huu,” amesema.
Vijana hao wa Jose Mourinho kwa sasa wanaelekeza nguvu zao
kwa ajili ya maandalizi ya kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu ya Uingeleza na
Mwishoni mwa wiki hii Juma Pili watafungua Ligi kwa Mtanange dhidi ya West Ham
Old Trafford.
No comments:
Post a Comment