uCHAGUZI tFF: Zamu ya Mayai Leo, amwaga sera zake, adai kurejesha dira ya soka nchini....#share
MGOMBEA urais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Ali Mayai amesema kuwa katika uongozi wake atahakikisha dira ya
mpira wa miguu inarejea katika mstari na kuiwezesha nchi kupata maendeleo
makubwa katika sekta hiyo.
Mgombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ali Mayai akizungumza na waandishi wa habari akinadi sera zake za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa TFF utakaofanyika Agosti 12, mkoani Dodoma, Kushoto ni mshambuliaji nyota wa zamani wa Klabu ya Simba, Zamoyoni Mogella.
Mayai amesema hayo leo alipokuwa
ananadi sera zake katika siku ya kwanza ya uzinduzi wa kampeni kuelekea
uchaguzi mkuu wa TFF utakaofanyika Agosti 12, mkoani Dodoma.
Amesema kuwa kwa
sasa hakuna dira ya mpira wa miguu na ndio chanzo cha kuwa na maendeleo duni ya
mpira kulinganisha na nchi zingine ambayo kwa sasa zinafaidi matunda baada ya
kuanzisha na kutekeleza dira hiyo.
“Kwa sasa wachezaji wengi wa Zambia
wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi, timu yao Taifa inafanya vizuri, Tanzania
ina wachezaji wengi wenye vipaji, lakini hakuna dira na kusababisha wao pia
kukosa dira katika fani yao,” alisema Mayai.
Alisema kuwa akiwa kama mchezaji,
ameweza kuona changamoto mbalimbali za mpira wa miguu na kuamua kugombea nafasi
iliyo ili kuzitatua na lengo lingine ni kujenga taasisi imara kwa kutumia
rasilimali zilizopo kwani tatizo si vipaji, bali ni aina gani ya uongozi
unaosimamia mpira wa miguu.
Wachezaji mbalimbali waliong’aa
katika medani ya soka hapa nchini, wamepigia chapuo mchezaji wa zamani wa timu
ya Taifa, Taifa Stars Ali Mayay kuchaguliwa katika nafasi ya urais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Mgombea huyo ambaye ni chaguo la
wachezaji wa zamani nchini aliungwa mkono na mshambuliaji nyota wa zamani wa
Klabu ya Simba, Zamoyoni Mogella ambaye alisema TFF inahitaji mtu kama
Mayay anayejua matatizo ya mpira wa miguu kwani ameucheza huo mpira.
Mogella ambaye enzi zake
alipewa jina la “Golden Boy” na “Morgan” alisema kuwa wanahitaji kuurudisha
mpira kwa wenyewe huku wakiwaomba wagombea kumchagua Mayay kwani ni wakati wa
mabadiliko kwa wadau wa soka nchini kwa kumchagua Mayay ambaye anavigezo vyote
katika masuala mbalimbali ya soka na uongozi.
“Mayay ni dira ya soka Tanzania,
amecheza soka kuanzia shuleni, katika hatua ya vilabu mpaka timu ya Taifa,
anajua nini cha kufanya ili kuleta maendeleo ya soka nchini,” alisema Mogella.
Mchezaji wa zamani wa Yanga Mohamed
“Adolph” Rishad naye alisema kuwa Mayay ni suluhisho sahihi kwa maendeleo
ya soka nchini na si wagombea wengine zaidi wachezaji wa mpira wa miguu
wametengwa katika soka na kukosa mwamko katika mchezo ambao wanaupenda.
Amesema kuwa kwa sasa Tanzania ina
matokeo mabaya katika soka la kimataifa ni kukosa uongozi wenye mapenzi ya
mchezo pamoja na Tanzania kuwa na vipaji vingi vya soka.
Na Karama Kenyunko Globu ya jamii.
No comments:
Post a Comment