sPORTS nEWS: Barcelona wamshika pabaya Neymar wa PSG....Sasa kumburuta Mahakamani...#share
Klabu ya Barcelona imesema kuwa inatarajia kuchukua hatua za
kisheria dhidi ya mchezaji wao wa zamani aliyetimukia klabu ya Paris Saint–German
(PSG) Neymar kwa kukiuka mkataba wake.
Barcelona wamebainisha kuwa wamedhamiria kumshitaki mchezaji
huyo ili awalipe fidia ya paundi milioni 7.8 kwa madai kuwa alikiuka mkataba
wake kwa kujiunga na PSG.
Mchezaji huyo wa kiamtaifa wa Brazili alikamilisha uhamisho
wake kutoka Barca kwenda PSG mapema mwezi huu dau la paundi milioni 198
lililohitajika kuvunja mkataba wake lilipotolewa.
Barca walijaribu kufanya kila kilichowezekana kumzua mchezaji
wao muhimu kuondoka, Kigogo wa La Liga Javier Tebas aliingilia kati lakini
hawakuweza kumzua Neymar kuwa mchezaji ghali zaidi duniani.
Hata hivyo, uhamisho huo mkubwa zaidi wa majira ya joto
umechukua sura mpya kwani Barcelona wanachunguza hasara ya euro milioni 8.5 zinazohusishwa
na malipo aliyopewa mchezaji huyo kama sehemu ya bonasi ya kuhuisha mkataba
wake aliposaini mkataba mpya mwaka jana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya Barcelona
imesema: "FC Barcelona imetoa madai dhidi ya Neymar kwa kukiuka mkataba wa
RFEF (Shirikisho la Mpira wa Miguu la Hispania) na imeshaifahamisha FIFA na
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ufaransa (FFF).
"Klabu inamdai mchezaji kurejesha fedha alizolipwa kama
sehemu ya bonasi kwani hajatimiza masharti ya mkataba wake. Kiasi cha euro
milioni 8.5, jumlisha riba ya 10%. Klabu imeitaka PSG kufidia kiasi hicho cha
fedha ikiwa mchezaji huyo hatawajibika kufanya hivyo.
"FC Barcelona imechukua hatua hii ili kulinda maslahi ya
klabu baada ya Neymar kuvunja mkataba wake na klabu ndani ya miezi michache tu
baada ya kusaini mkataba mpya hadi 2021."
Neymar ambaye alimwaga wino kusaini mkataba wa miaka mitano
Camp Nou 2016, ameanza maisha mapya ya Ligue 1 kwa kufunga mabao matatu na
kutoa pasi ya mabao matatu zaidi katika mechi zake mbili za kwanza.




No comments:
Post a Comment