sPORTS nEWS: Haruna Niyonzima hatimae ametua kwa ajili ya kuzinduliwa na wana Msimbazi Simba SC siku ya 'Simba day'
Wiki iliyopita uongozi wa klabu ya Simba kupitia Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari wa klabu hiyo, Haji Manara ulithibitisha kuwa ni kweli umsajili Haruna Niyonzima baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika.
Usiku wa jumapili ya Agosti, 6 mchezaji Haruna Niyonzima amewasili nchini tayari kwa ajili ya Simba Day itakayofanyika jumanne ya Agosti, 8 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo atakuwa mmoja wa wachezaji ambao watatambulishwa siku hiyo.
Pamoja na Niyonzima wachezaji wengine ambao wamewasili jumapili usiku ni Emmanuel Okwi na Nicholas Gyan.
Credit: Mo Blog.
No comments:
Post a Comment