sPORTS nEWS: Hazard, Kante, Sanchez na Kane kuchuana na Messi, Ronaldo kugombea uchezaji bora FIFA...#share

Harry Kane, Eden Hazard, N'Golo Kante and Alexis Sanchez wametajwa katika orodha ya wachezaji wanaowania zawadi ya mchezaji bora wa Dunia.

Wachezaji hao wa klabu ya Chelsea Eden Hazard na N’Golo Kante na Mshambuliaji wa Tothenham Harry Kane n mshambuliaji wa klabu ya Arsenal wameorodheshwa katika orodha ya wachezaji wanaowania mchezaji bora wa kiume wa FIFA kwa mwaka 2017.

Wachezaji hao wanaungana na wachezaji na Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic and Neymar katia orodha ya wachezaji 24 ambapo mshindi atatangazwa mwezi Januari.

Eden Hazard amekuwa amewekwa katika orodha hiyo kutokana na kufanikiwa kufunga magoli 16 na kufanya vizuri ndani ya jezi ya Chelsea na kuisaidia kupata ubingwa msimu uliopita.

Huku mchezaji mwenzake Kante, pia akichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Chelsea mwaka mmoja baada ya kufanya hivyo akiwa na klabu ya Leicester kwa kuchukua ubingwa wa ligi ya Uingereza.

Mshambuliaji wa Totteniham Harry Kane amefika hapo kwa kufanya vizuri msimu uliopita kwani alifunga magoli  29 na kuisaidia klabu yake kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi lakini pia ndiye mchezaji aliyechukua kiatu cha dhahabu.

Wakati Sanchez, alimaliza msimu wa  2016-17 kwa kuchukua ubingwa wa  FA, lakini pia laifanikiwa kufunga magoli  24.

The Fifa Best Men's Player 2017 shortlist

Pierre-Emerick Aubameyang, Leonardo Bonucci, Gianluigi Buffon, Dani Carvajal, Cristiano Ronaldo, Paulo Dybala, Antoine Griezmann, Eden Hazard, Zlatan Ibrahimovic, Andres Iniesta, Harry KaneN'Golo Kante, Toni Kroos, Robert Lewandowski, Marcelo, Lionel Messi, Luka Modric, Keylor Navas, Manuel Neuer, Neymar, Alexis Sanchez, Luis Suarez, Arturo Vidal.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search