bAD nEWS pOLISI: Mwanza, mtu mmoja akutwa ameuawa, Kamanda wa Polisi DCP: Ahmed Msangi awataka wananchi kufika kituoni kumtambua...#share
TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 17.08.2017
KWAMBA TAREHE 16.08.2017 MAJIRA YA SAA 17:30HRS KATIKA MTAA
WA KITANGIRI KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA
MWANAMKE JINA BADO HALIJAFAHAMIKA.
ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA 40 HADI
45 AMEKUTWA AKIWA AMEUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA NA MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE
PAGALA HUKU UKIWA UMEFUNGWA KWENYE MFUKO WA SANDARUSI NA KUZUNGUSHIWA NGUO
ALIZOKUWA AMEVAA MAREHEMU, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI MWILI WA MAREHEMU ULIWEZA KUONEKANA MAHALI HAPO BAADA
YA WATOTO WALIOKUWA WAKICHEZA ENEO HILO KUONA KIFURUSHI KILICHOTUPWA KWENYE
PAGALA NDIPO WALITOA TAARIFA KWA MAMA YAO.
AIDHA MAMA HUYO BAADA
KUFIKA NA KUONA KIFURUSHI HICHO NI MWILI WA BINADAMU ALIPATA MASHAKA KISHA
ALITOA TAARIFA KWA UONGOZI WA MTAA NA BAADAE WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI.
IMEONEKANA MWILI WA MAREHEMU HAUKUWA NA JERAHA LOLOTE, BALI
UCHUNGUZI WA AWALI UNAOSHE KUWA WAUAJI WALIMUUA KWA KUMZIBA PUNZI KISHA KWENDA
KUMTUPA KWENYE PAGALA ENEO AMBALO SI RAHISI MTU, BASKELI AU PIKIPIKI
KUPITA.
PIA INAONEKANA MAREHEMU ALIKUWA AKISUMBULIWA NA UGONJWA WA MATENDE
KWENYE MGUU WAKE WA KUSHOTO.
POLISI WANAENDELEA NA UPELELEZI NA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU
WALIOHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGENE NA MAUAJI YA MWANAMKE HUYO. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA
UTAMBUZI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI
AHMED MSANGI ANAPENDA KUWAELEZA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA KWAMBA KAMA KUNA MTU
YEYETO AMBAYE AMEPETOLEWA NA NDUGU YAKE AU JIRANI ALIYEKUWA AKISUMBULIWA NA
MARADHI YA MATENDE AFIKE KITUO CHA POLISI, ILI AWEZE KUPELEKWA HOSPITALI YA
BUGANDO ILI AWEZE KUUTAMBUA MWILI WA NDUGU YAKE, WAKATI AMBAPO JESHI LA POLISI
LINAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA KIFO HICHO.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
No comments:
Post a Comment