sPorTS nEWS: Neymar awazodoa wanaotolea macho 'mshiko wake' asema "mataji ninayo mengi, nimefuata changamoto PSG.." #share

Mshambuliaji wa Brazil Neymar amesema kuwa alihitaji changamoto mpya , wakati anapojiunga na klabu ya PSG kutoka Barcelona kwa kitita kilichovunja rekodi ya uhamisho cha (£222m).




Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alishinda mataji saba muhimu katika misimu yake minne katika uwanja wa Nou Camp ikiwemo taji la klabu bingwa mara moja na lile la La Liga mara mbili.

Amesema kuwa babake Neymar Sr alimtaka kusalia Barcelona.

''Nimeshinda mataji yote niliohitajika kushinda'' ,alisema Neymar ambaye atapokea mshahara wa (£40.7m) kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitano.

Akiandika katika mtandao wake wa Instagram, aliongezea: Nimeshinda mataji yote ambayo mchezaji soka anafaa kupata.

''Nimeishi maisha ambayo siwezi kusahau, lakini mchezaji anahitaji changamoto''.
''Na kwa mara ya pili katika maisha yangu, nitaenda kinyume na matakwa ya babangu''.

Uhamisho wa Neymar umevunja rekodi ya awali iliowekwa na Paul Pogba aliporudi kuichezea Manchester United kutoka Juventus kwa kitita cha £89m mnamo mwezi Agosti 2016.

Mshahara wake wa £782,000- kwa wiki unamaanishi kuwa PSG itamlipa £400m.

Neymar anatarajiwa kuzinduliwa mbele ya mashabiki wa PSG katika uwanja wa Parc des Princes siku ya Jumamosi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search