bREAKING nEWS: Mahakama Kuu yatupilia mbali pingamizi la kuapishwa Wabunge wapya wa CUF.. #share
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017 imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofutwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba ya kutaka wabunge wateule 8 wasiapishwe na Bunge.

Uamuzi huo, umetolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambaye amesema ametupilia mbali pingamizi hilo la zuio la kuapishwa kwa Wabunge hao 8 na kwa mantiki hiyo, Wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao wanaweza kuapishwa.
Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na waliokuwa wabunge wanane wa CUF kutaka wabunge wateule wasiapishwe. pic.twitter.com/w9gBMDpDhj— Swahili Times (@swahilitimes) August 4, 2017
No comments:
Post a Comment