sPORTS nEWS uLAYA: Wakati jioni hii Manchester United ikitarajia kushuka dimbani dhidi ya West Ham United, Neville hana imani na Lukaku...#share
Gary Neville bado ameonyesha kuwa na wasiwasi kwa mshambuliaji Mpya wa Klabu ya Mancester
United Romelu Lukaku kama anauwezo wa kufanya vizuri katika mechi kubwa.
“Romelu Lukaku lazima awe mchezaji ambaye anatakiwa kuisaidia
Manchester United kushinda katika michezo migumu na mikubwa Old Trafford msimu
huu,” amesema Neville.
Lukaku alijiunga na Manchester United akitokea
Everton kwa £75 million Julai mwaka huu na kufanikiwa kufunga goli kwenye
mechi dhidi ya Real Madrid katika kombe
la ikikombe cha ligi Ulaya Jumanne iliyopita (Super Cup).
Mbelgiji huyo alifunga magoli 25 msimu uliopita akiitumikia
klabu ya Everton huku akiwa ni mpachika nyavu wa pili nyuma ya Mshambuliajia wa
Tottenham Harry Kane katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu.
Lakini Neville bado amekuwa na maswali dhidi yake kwani
amekuwa akimtazama kwa ukaribu tangu alipowasili nchini Uingereza mwaka 2011.
“Wasiwasi wangu dhidi
yake ni kwamba nimekuwa nikimtazama kwa miaka kadhaa iliyopita akicheza katika
mechi kubwa na kwa wakati fulani sidhani kama amaweza fanya vizuri vya
kutosha,” Neville amesema hayo Sky
Sports.
No comments:
Post a Comment