tETESI zA uSAJILI uLAYA: Martial aichomolea Inter Milan, ataka kubaki kwa Malkia...#share

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester United Anthony Martial amekataa kujiunga na klabu ya Inter Milan, mshambuliaji huyo anataka kubaki katika ligi ya Uingereza (Premier  stay).


Inter imeulizia mshambuliaji huyo wa Kifaransa kuwa sehemu ya dili la uhamisho wa Ivan Perisic kwenda Manchester United.

Klabu hiyo ya San Siro imehitaji kiasi cha sh.  £48m pamoja na Martial kwa mkopo lakini kwa sasa inadaiwa kuwa mchezaji mwenyewe hataki kuhamia ligi ya Serie A.

Mwandishi wa habari wa Italian Tancredi Palmeri ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Martialkwa sasa amekataa pendekezo la Inter. Anependelea kubaki katika  Premier kama inawezekana,”.

Licha ya kwamba Martial hayupo tayari kwa uhamisho huo, Perisic anaweza kukamilisha uhamisho wake kwenda Old Trafford.

Inter na United wamekuwa katika misuguano ya kukubaliana ada ya uhamisho ya Mkoreshia huyo tangu suala hilo lianze kuzungumzwa miezi kadhaa sasa.
Inaarifiwa kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita Ed Woodwood alifungua mazungumza ya uhamisho wa Perisic kwa kiasi cha  £48m.

Lakini kocha wa Inter Milan  Luciano Spalletti ameendelea kusisitiza kuwa mchezaji huyo anataka kubaki.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search