Wanachama TEF nako 'washikana mashati' walaani maamuzi ya Viongozi wao kuondosha 'marukufuku' kwa RC Makonda 'kinyemela'.. #share

WANACHAMA wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), wametoa onyo kwa uongozi wa jukwaa hilo kwa kitendo cha kutoa uamuzi wa kuandikwa na vyombo vya habari taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam bila kuwashirikisha.


Onyo hilo limetolewa kupitia katika taarifa yake kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Mkutano Mkuu Maalum wa TEF, Walles Maugo kwa niaba ya wajumbe wa jukwaa hilo baada ya kikao cha dharura kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Maugo amesema baada ya wajumbe kukutana na kujadili walibaini kuwepo kwa kasoro kubwa wakati wa mchakato wa kurejesha uhusiano wa kikazi kati vyombo vya habari na mkuu huyo wa mkoa.

Amesema jukwaa kwa kauli moja limeutaka uongozi kutorudia tena kosa hilo la kiuwajibikaji, kikanuni na kitaratibu.

Pia uongozi umetakiwa kuhakikisha kila panapotokea suala kama hilo ambalo lilifanyiwa uamuzi na mkutano mkuu wa TEF kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kihabari, unarejeshaje kwa wanachama kabla ya hatia za mwisho kuchukuliwa,” alisema

Amesema viongozi wa TEF ambao walitoa maamuzi hayo walikiri kosa na kuomba radhi kwa kuitisha mkutano wa waandishi wa habari kabla ya kupata idhini ya mkutano mkuu hali ambayo inajenga taswira mbaya ya kiuwajibikaji kwa jukwaa.

Maugo amesema TEF inawahakikishia wanahabari na wananchi kuwa litaendelea kutimiza wajibu wake wa kitaaluma na halitasita kuchukua hatua stahiki kwa kiongozi au mtu yeyote atakayeonekana kutishia usalama wa wanahabari, uhuru wa uhariri na vyombo vya habari.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search