Askali Poilisi Amuua Mkewe kwa Risasi Kisha na Kisha Akajifyatulia Mwenyewe..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

ASKARI Polisi Stephen Mungai Kinuthia wa jimbo la Nakuru nchini Kenya amemuua mkewe kwa kumpiga risasi kichwani na kisha kujiua mwenyewe mbele ya mtoto wao.
Kinuthia ambaye alikuwa skari polisi wa kituo cha Molo, amempiga risasi mpenzi wake huyo mara tatu kwa kutumia bunduki ya AK47 wakiwa nyumbani kwao.

Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mlinzi wa eneo hilo amesema walisikia kelele za watu wakilumbana, na walipokuwa wakikimbilia kujua kulikoni walisikia milio ya risasi na kisha kukawa na ukimya.

Majirani wa eneo hilo wamesema walisikia kelele za mtoto akilia kwa sauti huku akisema baba anamuuwa mama.

OCPD wa Nakuru Joshua Omukatta amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, huku miili ya marehemu wote ikiwa imepelekwa katika hospitali ya serikali ya Nakuru.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search