Aveva, Kaburu Bado Hakijaeleweka Mahakamani....#share

KESI inayowakabili viongozi wa juu wa klabu ya Simba, Evans Aveva na Geofrey Nyange 'Kaburu' imehairishwa hadi Septemba 27 mwaka huu, huku upelelezi wao ukiwa umekamilika na jalada lao kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Hayo yamebainishwa leo na Wakili wa serikali, Nassoro Katuga na kumueleza Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Victoria Nongwa  kuwa upelelezi wa awali wa kesi hiyo umekamilika na jalada limepelekwa kwa DPP ili aweze kulipitia na kuona kama umekamilika au laa

Mara baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa ameamuru kuahirishwa kwa kesi hiyo na kusikilizwa tena hadi Septemba 27 mwaka huu.

Viongozi hao walikamatwa na TAKUKURU miezi michache iliyopita wakikabiliwa na mashtaka matano ambayo mawili kati ya hayo ni ya kutakatisha fedha.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search