Siku Kadhaa Baada ya Kuachiwa Huru Mfanyabiashara Yusuf Manji Ameripoti Tena Mahakamani Leo....#share

KESI ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Mfanyabiashara Yusuf Manji inatarajiwa kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Hivyo kesi hiyo itaanza kusikilizwa kuanzia Septemba 25 hadi 27 mwaka huu kwa kusikiliza ushahidi  wa upande wa utetezi wa Mfanyabiashara huyo.

Wakili wa Serikali Mkuu, Timony Vitalis amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa, kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini yeye ana safari akidai kuwa leo mchana anatarajia kusafiri, hivyo ushahidi wa kesi hiyo ukianza kusikilizwa atachelewa.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha alimuuliza Manji kwa nini amechelewa kufika Mahakamani, ambapo Manji alijibu alikuwa eneo la karibu hivyo alisubiri aitwe na Wakili wake.

"Nisamehe sana Mheshimiwa, niliambiwa umetoka, hivyo nilisubiri Wakili anipigie simu kama ungerudi,"

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi September 25-27, 2017 kwa ajili ya kusikilizwa mfululizo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search