Baada ya Kubenea, Zitto, na Lema, Spika Ndugai aingia 18 za Peter Msigwa.....#share
MBUNGE wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Peter Msigwa amesema Spika Job Ndugai hana sifa ya kuwa
kiongozi wa kusimamia nidhamu ndani ya bunge.
Msigwa amebainisha hayo leo jijini Nairobi nchini Kenya alipokwenda kwa ajili ya kumjulia hali Mbunge
wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu aliyelazwa kufuatia shambulio la
kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Itakumbukwa hivi karibuni Lissu alipigwa risasi zaidi ya 30
akiwa mjini Dododoma kwa ajili ya mikutano ya Bunge inayoendelea hali
iliyopelekea kusafirishwa kwa matibabu nchini Kenya.
"Ninaomba mumuogope Mungu kwa sababu tunaleta mchezo na
maisha ya Watanzania, mnataka kutunyamazisha ili tusiseme. Tutasema mpaka
mwisho wetu kwa sababu uhai wetu na usalama wa taifa letu umetishiwiwa kwa
kiwango cha juu sana lakini Mhe.
Ndugai wewe kama spika unasifa gani ya kutuambia sisi tuwe na adabu ndani ya bunge wakati wewe mwenyewe kipindi cha kampeni ulionekanaa ukipiga watu hadharani na fimbo, ulitakiwa uwe gerezani na siyo kutusimamia nidhamu ndani ya bunge", amesema Msingwa.
Ndugai wewe kama spika unasifa gani ya kutuambia sisi tuwe na adabu ndani ya bunge wakati wewe mwenyewe kipindi cha kampeni ulionekanaa ukipiga watu hadharani na fimbo, ulitakiwa uwe gerezani na siyo kutusimamia nidhamu ndani ya bunge", amesema Msingwa.
Aidha amedai kuwa Ndugai ni adui wa usalama wa Taifa nchini
kutokana na kulisababisha bunge kuwa dhaifu kwani serikali imemteka kiasi cha
kupokea maagizo toka serikalini hivyo kuufanya mhimili wa bunge kuwa butu na
kushindwa kuisimamia.
“Nasema haya kwa ujasiri mkubwa sina kitu cha kuogopa tena
kama ndugu yetu ameshapigwa risasi na tumeshaambiwa tunaofutwa ni sisi hivyo
hatuna cha kuogopa kusema jambo lolote", amesisitiza Msigwa.
Pia Mbunge huyo
ameongeza kutokana na tabia za Spika huyo wakati mwingine wanashindwa hata kuwaambia watoto wao kuwa ni
kiongozi wao wa bunge kwani mekuwa wakiwatishwa, wakifukuzwaa paoja pamoja na kupigwa
pingu huku akisisitiza kuwa yupo tayari kufukuzwa bungeni lakini hatoweza kukaa
kimya.
Na Abrahama Ntambara
No comments:
Post a Comment