News: Mbunge wa Kawe Halima Mdee ataja sababu za kukataa wito wa kuripoti kwa DCI.. #share

MBUNGE wa Jimbo la Kawe jijini Dar es salaam Halima James Mdee amesema hajaenda kuripoti kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kama alivyotakiwa kutokana na kwamba hajaitwa kwa njia rasmi.

Mbunge huyo Machachali ametoa kauli hiyo leo akizungumza na kituo kimoja cha Luninga nchini.

Mdee amesema kuwa DCI alipotaka kuripoti kwake alitoa tangazo la ujumla, lakini yeye binafsi hakupewa wito wowote, hivyo hawezi kwenda kutokana na taarifa hiyo.

“Mimi nimesikia tangazo la ujumla, wakiniita in personel Halima njoo nitaenda na hakuna popote kwenye kauli yao iliposema Halima Mdee njoo, lakini siwezi kwenda kwa ‘general statement’, amesema Mdee

Itakumbukwa juzi Jeshi la Polisi nchini liliwataka watu wote waliopost kwenye mitandao ya kijamii kuhusu askari wao aliye nchini Nairobi wakimuhusisha na kumfuatilia Tundu Lissu nchini Kenya kwenye matibabu kuripoti wenyewe kwa DCI.

Aidha watakiwa kufanya hivyo kwa hiari yao, kabla ya kitengo cha sheria za makosa ya mtandaoni hakijawachukulia hatua zaidi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search