Benki ya Afrika-Tanzania yazindua huduma ya 'SWAHIBA Mobile App' kurahisisha huduma za kibenki...#share
BENKI ya Afrika-Tanzania (BOA) imezindua programu ya benki
inayoitwa ‘SWAHIBA Mobile App’ ambayo itawawezesha watumiaji wa Banki hiyo
kufurahia huduma kamili za benki kwa njia ya simu kupitia mtandao wowote wa simu muda wote.
Vingozi wa BOA wakifurahia jambo baada ya uzinduzi wa huduma ya 'SWAHIBAMobile App' leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo Dar es Salaam, Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za E-Banking wa benki hiyo Emmanuel Mshindo, amesema programu
hiyo itawarahisishia wateja kutumia huduma
za kibenki katika simu kwani inasifa zinazowapa wateja uwezo wa kufikia zao
binafsi na za kibiashara kwa wakati mmoja.
“Huduma zinazopatikana kwenye program hii ni huduma za
kuhamisha fedha, huduma za hundi, maombi ya mkopo wa papo hapo, malipo ya bili,
huduma za utoaji fedha kwenye ATM bila kadi, kuongeza muda wa maongezi, usajili
binafsi wa mobile banking na huduma za e-chama pamoja na nyingine nyingi,” amesema
Mshindo.
Aidha amesema zaidi ya hayo, SWAHIBA Mobile App itakuwa na
uwezo wa kutumiwa na mtu yeyote hata ambaye siyo mteja wa benki hiyo. Ametaja huduma
ambazo mteja mwingine anaweza kupata ni huduma za Bank Of Africa, Maombi ya
Mikopo, Matawi ya benki na ATM, benki katika mtandao ‘internent banking’ na
viwango vya ubadilishaji fedha za kigeni.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa BOA, Ammishaddai Awusu-Amoah, amesema
wanajivunia kuanzisha program hiyo ya benki kiganjani katika wakati huu ambapo
benki yao inaadhimisha miaka 10 ya biashara nchini.
“Uzinduzi wa SWAHIBA Mobile App ni alama ya shukrani zetu kwa
wateja, jamii na wadau wote katika kipindi cha miaka 10 ya kazi nchini,” amesema.
“Huduma hii pia inakuja kutia msisitizo wa ahadi yetu ya
kuweka mapendekezo ya wateja wetu kwanza na kuwaongezea uzoefu wa kidigitali
zaidi katika ukuaji wa sayansi na teknolojia. Pia inathibitisha uamuzi wa benki
wa kujenga uwepo wake wa kidigitali na kukidhi mahitaji ya haraka ya wateja
wetu,” ameongeza Awusu-Amoah.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maxcom Afrika Jimson Kasatti
amesema huduma hiyo pia inapatikana kupitia Max Malipo na kuongeza kuwa wapo
mbioni kujiunga na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ili kuwa wezesha wananchi
kununua na kumiliki hisa kutoka Max Malipo.
Na Abraham Ntambara








No comments:
Post a Comment