Baada ya Spika Ndungai, Lema 'amuamshia dude' Humphrey Polepole,.. asema tamko la kumpongeza'Turky' ni la (...) #share
BAADA ya juzi Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kumshambulia Spika wa Bunge Job Ndugai kuwa anapotoha juu ya taarifa za matibabu ya Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu
Lakini pia kwa kushindwa kulisimamia Bunge wakati huu ambao Lissu yuko jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu.
Mbunge huyo amegeuzia mashambulizi kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole kwa kumwambia kuwa ametoa tamko la kijinga.
"Humphrey Polepole, nimeona tamko la kijinga lililojaa uongo. Hata hivyo linafanana na wasi wasi wa fikra zako," amesema Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Aidha shambulizi hili la lema dhidi ya Polepole limekuja baada ya Polepole kumpongeza Mbunge wa Mpendae CCM kukisaidia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukodi ndege iliyomsafirisha Kiasi kwa ajili ya matibabu.
"Tanzania ni moja, ni nchi yetu sote, na itajengwa na wazalendo, wenye utu, mshikamano na upendo. Tutende wema, hongera Mwana CCM Mr. Wote, " amesema Polepole kwenye ukurasa wake wa Twitter.

No comments:
Post a Comment