Watu wasiojulikana wamkata mapanga dereva wa Mbunge Heche... #share

DEREVA wa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche amevamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na kukatwa mapanga akiwa Tarime mjini majira ya saa 2 usiku na inaelezwa hali yake siyo nzuri.


Mbunge John Heche amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kutokana na taarifa alizopata kupitia Katibu wake, Mrimi Zablon ambaye amekiri Dereva huyo anayefahamika kwa jina la Suez Daniel Maradufu ni kweli amepata shambulio hilo na sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu.

Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, SACP Henry Mwaibambe alipotafutwa kwa njia ya simu na Mwandishi wetu amesema yupo kwenye kikao na akimaliza atatoa ripoti kamili.

Dereva huyo amelazwa katika hospitali ya Bomani Tarime mkoani Mara.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search