Breaking: Kila unachopaswa kufahamu kuhusu maamuzi aliyoyafanya JPM leo kwa aliyekuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahim Hamis Juma.. #share

JAJI PROF.IBRAHIM HAMISI JUMA,NI MWANAZUONI NGULI ALIYETUKUKA
JAJI PROF. IBRAHIM KITAALUMA ANA

1.Bachelor of Laws,UDSM
2.LLM,UDSM
3.Specialist,Law of Sea,LLM Ghent University,Belgium
4.Master of Laws(international Human Rights Law) Raoul Wallenberg University,Lund,Sweden wanaojua hiki ni moja ya vyuo bora zaidi vya Haki za Binadamu Ulaya
5.PhD,Law of sea,Ghent University,Belgium

Jaji Prof Ibrahimu ni mwanazuoni mbobevu katika sheria za Bahari,ni kati ya wasomi wachache walioko Tanzania wenye utaalamu huo wa Sheria za Bahari akiwemo Prof Mahalu na Prof. Nasila Rembe kwa wale waliopitia vyuoni hasa upande wa sheria za Bahari,Haki za Binadamu,Sheria za Wakimbizi na Sheria za Mazingira wanamtambua Prof Ibrahimu kwa Machapisho na maandiko yake ambayo yanatumika na kila mwanafunzi.

Weledi wake katika Sheria utaleta mwanga mpya katika muhimili huu wa Mahakama ameapishwa kukaimu nafasi ya ujaji Mkuu wakati Taifa likikabiliana na vita dhidi ya Ubadhirifu,uhujumu uchumi vikiwemo ujangili,Rushwa na ukiukwaji wa Maadili kwa baadhi ya watendaji wa Umma kwa Kifupi Mtihani alionao ni kurejesha imani  kwa wananchi juu ya watendaji wa Mahakama kuzingatia Sheria,Haki na Wajibu,Pongezi Jaji Prof Ibrahim Juma...

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search