BREAKING: Mahakama Kuu yatengua matokeo ya Uchaguzi Mkuu Kenya yaliyompa ushindi Kanyatta...#share

Mahakama Kuu Kenya imebatilisha matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa
Kenya uliofanyika August 8, 2017 ambao ulimpa ushindi Uhuru Kenyatta dhidi ya Raila Odinga na kutaka kuandaliwa
uchaguzi mwingine ndani ya siku 60.
Mahakama hiyo imeeleza kuwa IEBC haikuandaa uchaguzi huru na wa haki ambapo Jaji
Mkuu David Maragaameagiza
uchaguzi haukuandaliwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria, hivyo matokeo yake ni
batili.
“Natangaza hapa kwamba Kenyatta
hakuchaguliwa na kutangazwa kwa njia inayofaa. Agizo linatolewa, kuagiza Tume
ya Uchaguzi kuandaa na kufanyisha Uchaguzi mwingine kwa kufuata Katiba na
Sheria katika kipindi cha siku 60.” – Jaji Maraga.
Hatua hiyo imekuja baada ya mgombea Urais kupitia Muungano wa
Upinzani NASA, Raila Odinga kufungua
kesi Mahakamani kupinga matokeo yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta ambaye alitangazwa mshindi na Tume Huru ya
Uchaguzi IEBC.
Kesi hiyo ilikuwa na Majaji Saba ambao wawili kati yao; Justice Jackton Ojwang’ na Njoki Ndung’u walisema Uchaguzi
huo uliendeshwa kwa misingi ya haki na huru.
Kwa uamuzi huo sasa Uhuru Kenyatta hatoapishwa kama Rais Mteule bali atasubiri
tena matokeo baada ya Uchaguzi utakaoitishwa ndani ya siku 60.
By
No comments:
Post a Comment