sPORTS nEWS: Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney ashikiliwa na Jeshi la polisi wa kosa la kuendesha.....#share

NAHODHA wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Uingereza Wayne Rooney anashikiliwa
na jeshi la Polisi nchini humo akiwa karibu na nyumbani kwake katika mji wa
Cheshire kwa kosa la kuendesha gari huku akiwa amelewa.
Kwa mujibu wa the Mirror, Rooney ambaye ni Mfungaji bora
wa muda wote wa Uingereza amekatwa usiku wa jana alipokuwa katika mtoko wake wa
jioni
Mshambuliaji huyo
mwenye umri wa miaka 31 inaaminika kuwa alipelekwa katika kituo kiudogo cha
polisi kilichopo kwenye mji wa Cheshire ambapo alihojiwa na maofisa wa polisi.
Chanzo kinasema kuwa :
'Maongezi yake yalikuwa hayaeleweki, mdomo wake ulikuwa mwekundu na wine pamoja
na macho yeke kuwa mekundu.
Tangu ajiunge tena na
klabu ya Everton Rooney amefunga magoli 2 katika michezo mitatu na alicheza pia
katika mchezo ambao klabu yake ilipoteza 2-0 dhidi ya Chelsea.
Rooney siyo mchezaji wa
kwanza wa kimataifa kusimamishwa na kukamatwa na polisi kwa kusa la kuendesha
gari huku amelewa.
Mwezi wapili mwaka huu
mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Roberto Firmino alifungiwa kuingia barabarni
kwa mwaka mmoja na kupigwa faini ya pauni Milioni 20,000 kwa kosa la jinsi
hiyo.
No comments:
Post a Comment