Breaking: Mbunge Zitto Kabwe Anashikiliwa na Jeshi la Polisi....Taarifa na Matukio360..#share
KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, na Mbunge wa Kigoma
Mjini Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi muda huu uwanj a wa ndege wa wa Julius Nyerere (JNIA),jijini Dar
es salaam wakati akitoka Kigoma.

Kwamujibu wa Afisa habari wa chama hicho Abdallah Khamisi
amesema Kwa sasa wanasheria wa chama wanafuatilia kujua sababu za kukamatwa
kwake.
Mbunge Zitto amekamatwa kufuatia agizo la Katibu Mkuu wa
Bunge Dk. Thomas Kashililah ambaye
jana aliagiza Mbunge huyo asakwe popote alipo ili apelekwe kwenye Kamati ya
Maadili ya Bunge.
Aidha kwa mujibu wa Dk. Kashililah ni kwamba Zitto alikwishapatiwa
barua ya kutakiwa kufika mbele ya Kamati hiyo lakini hakufanya hivyo.
Itakumbukwa pia jana Mbunge wa Ubungo Sued Kubenea alikamatwa na Jeshi la Polisi na kisha leo Alfajiri akasafirishwa kenda mjini Dodoma.

Na Abraham Ntambara

Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment