Bavicha Watangaza Maandamano...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360...#share
BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Bavicha) Mkoa wa Kagera limetangaza kuandaa maandamano ya amani kulaani tukio
la kushambuliwa kwa risasi Mwanasheria Mkuu wa chama chao, Tundu Lissu
aliyeshambuliwa Septemba 7, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Bavicha Manispaa ya Bukoba, Ishengoma
Audax alisema licha ya kuandamana watakwenda katika Hospitali ya Rufaa Bukoba
kuchangia damu.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa
Kagera, Francis Rutta amesema wameamua kuandamana kulaani kushambuliwa kwa
Lissu na kuvitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinawakamata na kuwatia mbaroni
wahusika.
“Tunafanya maandamano ya amani hivyo hatutegemei polisi
kuzuia maandamano yetu kwa kuwa ni ya amani.
“Lakini tunaunga mkono uamuzi wa Brlaza Kuu la Taifa Bavicha
linaloongozwa na Mwenyekiti Patrobas Katambi,” amesema.
Amesema wamekuwa wakishangazwa na hatua ya polisi kuwazuia
wananchi kumuombea Tundu Lissu ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa makada wa chama
chao waliovaa fulana zenye ujumbe wa kumuombea.
Amesema huo ni ukiukaji mkubwa wa demokrasia.
No comments:
Post a Comment