bREAKING nEWS: Chadema yatoa 5 kwa Mahakama Kenya kufuta ushindi wa Kenyatta, Pia yashauri mambo 3 kufanyika nchini ili kuiga nyendo za Kenya...#share

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mahakama ya Juu ya Kenya (The Supreme Court of Kenya) imeweka
historia Afrika. Baada ya kushuhudia Mahakama ikiendeshwa kwa uhuru na uwazi
huku ikitangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya nje na ndani ya Kenya.
Leo imehitimisha kesi kwa kutoa hukumu ya kihistoria na
ambayo imeweka funzo kubwa na muhimu katika ukuaji na uimarishaji wa demokrasia
katika Bara la Afrika.
Mahakama ya Juu ya Kenya imeagiza uchaguzi wa Rais ufanyike
upya ndani ya siku 60 kama ambavyo Katiba ya Kenya inataka.
Hukumu hii imetolewa kutokana na uhuru wa Mahakama ya Kenya
ambao umetokana na misingi iliyowekwa na Katiba na Sheria za nchi hiyo.
Kutokana na historia hiyo ya kipekee iliyoandikwa na majirani
zetu wa Kenya kupitia Mahakama ya Juu, CHADEMA tunashauri ifuatavyo;
1. Ni wakati mwafaka sasa Tanzania tukarejea katika mchakato
wa kupata Katiba Mpya na yenye kuweka taasisi imara.
2. Rais John Magufuli amdhibitishe Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania kwani hadi sasa amekaa muda mrefu akikaimu tangu ateuliwe kushika
nafasi hiyo. Hii itasaidia kuufanya mhimili huu uweze kuwa huru na kujisimamia
katika shughuli zake za kutafsiri sheria na kutoa haki.
3. Katiba Mpya ambayo Watanzania wanaitaka iweke kipengele
cha matokeo ya urais baada ya uchaguzi mkuu, kuhojiwa mahakamani.
4. Katiba Mpya iunde Tume Huru ya Uchaguzi na ambayo pia
itaweza kushtakiwa mahakamani pale ambapo kuna tuhuma au madai ya uchaguzi
kuharibiwa au kuingiliwa kinyume cha taratibu za uchaguzi huru na haki.
Hukumu ya Mahakama ya Juu ya Kenya ituamshe Watanzania kwa
pamoja tudai Katiba mpya na ambayo itaweka misingi imara ya taasisi zetu nchini
na hatimaye tuweze kuwa na chaguzi huru na za haki.
Mwisho tunawatakia Wakenya uchaguzi mwema wa marudio baada ya
hukumu hiyo ya kihistoria ambayo imedhihirisha uimara mkubwa wa demokrasia na
utawala bora.
Hiyo ni ishara na funzo kubwa linaloonesha ukomavu wa taasisi
zilizoundwa kikatiba.
Imetolewa leo Ijumaa, Septemba 01 Septemba 2017.
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje
No comments:
Post a Comment