Chiana Yaipatia Tanzania Msaada wa Sh. bilioni 29.4 kwa Ajili ya Miradi ya Maendeleo..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
SERIKALI ya Tanzania imepokea msaada wa Sh bilioni 29.4 kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya utekelezaji na uboreshaji katika sekta ya elimu, utalii na michezo.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam baada kukamilsha taratibu za upokeaji msaada huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amesema msaada huo umegawanywa katika awaamu tatu na kubainisha ya kwanza kiasi cha Sh bilioni 22.4 zitumika kujenga Chuo kipya cha Mafunzo ya Ufundi, mkoani Kagera kitachokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 kwa wakati mmoja.
Aidha, amesema fedha hizo zitajenga madarasa 19, karakana 9, Jengo la Utawala, mabweni ya wanafunzi pamoja na nyumba za walimu wa chuo hicho.
" Tunawashukuru Serikali ya China kwa msaada huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapa ujuzi utakaowasaidia kupata fursa za kujiajiri na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira," amesema Dotto.
Amebainisha kuwa awamu ya pili Sh bilioni 6.7 zitatumika kwenye ukarabati n maboresho ya Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 kwa wakati mmoja na kwamba zitanununulia vifaa vya michezo na vifaa vya teknolojia.
Katibu Mkuu huyo amesema tangu China ilipokamilisha ujenzi wa uwanja imekuwa ikiendelea kusaidia kuufanyia marekebisho na ukarabati mara inapohitajika.
Amefafanua kuwa Sh. milioni 300 zitaelekezwa kwenye Ujenzi wa Kituo cha Utalii wa Jiolojia lengo likiwa kuongeza idadi ya watalii wanaotoka China na mataifa mengine pamoja na kuliingiza taifa fedha za kigeni.
Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China nchini, Gou Haodong amesema nchi hizi zina uhusiano wa karibu tangu za Mwalimu Julius Nyerere na kwamba itaendelea kutoa misaada katika miradi mbalimbali yenye lengo kuisaidia nchi kiuchumi na kijamii.
Na Hussein Ndubikile
No comments:
Post a Comment