Baada ya Serikali ya JPM Kufungia Gazeti la Raia Mwema.. Hashimu Rungwe Aibuka na Kuichana Serikali..#share
WAKATI ndani ya siku kumi serikali ya Rais ya John Magufuli
ikiwa ni teyari imeyafungia magazeti mawili ndiyo naweza kusema baada ya leo
serikali kutangaza kulifungia kwa siku 90 gazeti linalotoka mara moja kwa wiki
la Raia Mwema kutokana na kuandika habari inayodaiwa kumchafua Rais
Magufuli.
Mbali na Gazeti hilo katika siku hizo, pia serikali hiyo
imetangaza kulifungia kwa miaka miwili gazeti la Mwanahalisi kutokana na
kuandika habari ambazo serikali inadai zinakiuka kanuni za uandishi wa habari.
Hatua hiyo imepingwa vikali na wanasiasa huku wakisema hatua
hiyo ni muendelezo wa serikali ya Rais Magufuli kuminya demokrasia .
Hashim Rungwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi
wa Umma ameumbia Mtandao wa Matukio360.blog, kuwa hatua ya serikali kulifungia
gazeti hilo imekiuka msingi ya haki za binadamu huku akitaja ni
mwendelezo wa ukandamizaji wa demokrasia hapa nchini.
“Huu ni muendelezo wa ukandamizaji wa demokrasia,ameaanza
kwetu wanasiasa,Leo wanataka kuwatisha wanahabari wasiandike habari
ambazo wa wao hawasipendi,”amesema Rungwe.
Rungwe ambaye alikuwa mgombea wa Urais kwenye uchaguzi mkuu
wa mwaka 2015 amesema kwa sasa kinachoonekana kwenye tasnia ya habari ni
serikali kujivika koti Uhariri wa habari.
"Sahivi serikali imekuwa mhariri wa habari,kama utaki
watu waandike habari si useme waandike za kukusifia wewe,akumbuke yeye ni baba
wafamilia lazima watu wamkosoe,"amesema Rungwe ambaye ni Wakili Msomi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Raia Mwema, Jenerali Ulimwengu amesema
wameambiwa sababu ya kusitishwa kwa gazeti hilo ni habari hiyo.
Ulimwengu amesema kwa sasa wanashauriana kuona ni nini cha
kufanya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya
Habari maelezo,Dk Hassan Abbasi kwa vyombo vya habari inasema serikali imefikia
hatua kulifungia gazeti la Raia Mwema kutokana kuandiika nukuu ya uongo kwa
Rais Magufuli.
Amesema toleo la namba 529 la terehe 27 semptemba hadi
Oktoba mwaka ilichapisha habari ya Uchambuzi inayosema “URAIS UTAMSHINDI JOHN
MAGUFULI”
“Makala hiyo ilisheheni nukuu za kutunga na
zisizo za ukweli zikimsingizia Rais John Magufuli ,Gazeti hili limeonywa
sana huko nyuma dhidi ya uandishi wake” Amesema
Kufungiwa kwa Gazeti hili kunakuja ni siku moja baada ya
wamiliki wa Gazeti la Mwanahalisi kutangaza kukimbilia Mahakamani kutaka Gazeti
hilo lifunguliwe.
Kufungiwa kwa Gazeti la Raia Mwema linakuwa ni miongozi mwa
magazeti zaidi ya 400 kufungia tangia Rais Magufuli aingie madarakani katika
miaka yake miwili,
Magazeti 400 hayo mengi yake yakifungiwa kutokana na
kutochapishwa kwa mada mrefu huku yaliobakia yakifungiwa kwa sababu inayotajwa
kuwa yanakiuka misingi ya uandishi wahabari.
No comments:
Post a Comment