Ecobenki Waja na Huduma ya Kidigitali ya Mobile Banking Masterpass na M-VISA...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360

BENKI ya Biashara Ecobank imezindua huduma ya kidigitali Mobile banking ya Masterpass na M-VISA ambayo itamwezesha mteja kufanya miamala mbalimbali kwa urahisi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jinni Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobenk Mwanahiba Mzee amesema benki hiyo imevunja historia ya kuwa wakwanza kuanzisha huduma hiyo nchini.

“Huduma hii siyo lazima mteja atumie Card ya benki bali unakuwa tu na applicationin ya Ecobenk Mobile kasha utaweza kupata huduma zote za kibenki, unaweza kulipia huduma za chakula, biashara na kadhalika,” amesema Mzee.

Naye Meneja Huduma za Kidigitali wa benki hiyo Philemon Tesha amesema kwa kutumia huduma hiyo unaweza kuhamisha Fedha kutoka akaunti moja kwenda nyingine ndani ya benki hiyo.

Aidha ameongeza pia unaweza kufanya miamala ya kifadha hadi nje ya nchi.

Akizungumzia faida ya Ecobenk Mobile amesema inamsaidia mfanyabiashara kufanya matumizi ya fedha Zaidi ya kiasi alichonacho mfukoni.
Na Abraham Ntambara

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search