TCRA Yawataka Wanachi Kufahamu Matumizi ya Sahihi ya Mitandao...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
MAMLAMA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka Wananchi
kuwa na ufahamu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kompyuta na Internent.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Meneja
wa Mawasiliano TCRA Semu Mwakanjala akizungumza na waandishi wa habari, amesema ufahamu huo utawasaidia kukabiliana uhalifu wa kimtandao.
Amesema wanatoa ushauri wa kitaaluma wa kukabiliana na
matukio ya kiusalama yanayotokea kwa lengo la kuzuia madhara.
“Tunawasihi watu wasijibu jumbe wanazopokea kwenye akaunti zao
za barua pepe au ujumbe mfupi bila kuhakiki uhalali wa taarifa” amesema Mwakanjala.
Hata hivyo amesema mtu hatakiwi kufungua Link anayotumiwa na
mtu asiyemjua bila kuhakiki ni kitu gani kilichotimwa.
Aidha amewatahadharisha watu waache kusambaza ujumbe wenye
uzushi, uchochezi na chuki kwani hatua kali zitachukuliwa.
Amesema watu waache kutungeneneza akaunti za mitandao kwa
lengo la kufanya utapeli na ulaghai na taarifa za uongo.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment