Gazeti Hili Nalo Laingia Mgogoro na Serikali...Je Kupigwa "Stop" Kama Gazeti la Mwanahalisi?..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
GAZETI la Raia Mwema ambalo linatoka mara moja kwa wiki liko mbioni kufungiwa ama kupewa onyo kali na serikali ya Rais John Magufuli  kutokana na kuandika kichwa cha habari kinachoelezwa kumchafua Rais.(Mtandao huu umedokezwa).

Gazeti la Raia Mwema ambalo linatoka kila jumatano na ni miongoni mwa Gazeti ambalo linaandika habari za uchunguzi zenye Makala mbali  za kisiasa na za kijamii.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa mtandao huu kutoka ndani ya habari maelezo ambaye amekataa kutaja jina lake kutajwa mtandaoni amesema toleo la Gazeti la Raia Mwema la jana tarehe 27 hadi  tarehe 2 ya mwezi wa kumi mwaka huu lilikuwa na habari yenye kichwa cha habari “URAIS UTAMSHINDA MAGAFULI’ ambapo kichwa cha habari hicho kinatajwa kumkashifu rais.
“Ujue bwana hawa watu habari ya jana imetushtua sana,wahariri wa gazeti hilo wameitwa hapa waje kujitetetea kutokana na habari ile,maana habari hii inamkashifu rais hawezi ukasema Urais utamshinda"
"wakati nchi ipo vizuri amani ipo mambo yanaenda kwahiyo hawa watu wamemkashifu rais kwahiyo wewe ngojea lolote kutoka serikali itakaloamua  ”amesema mtoa taarifa wetu.
Taarifa hii inakuja ikiwa ni wiki moja kupita baada ya serikali kulifungia  kwa miaka miwili gazeti ambalo linatoka mara moja kwa wiki la mwanahalisi  kutokana na kuandika habari ambazo zizotajwa kuwa ni za uchochezi.
Mbali na Gazeti hilo kwa kipindi cha Miaka miwili tangie Rais Magufuli aingie madarakani ni teyari serikali  imeyafungia magazeti Zaidi ya 400 kutokana  na magazeti hayo kutochapishwa kwa mda mrefu huku baadhi yao yakifungiwa kutokana kuandika habari zinadaiwa kuwa ni za uchochezi.
Mtandao huu ulipomtafuta  Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo ,Dk Hassan Abbas kuzungumzia taarifa hizo, jitihada za kumpata hazikufanikiwa kutokana na  simu yake kutopatikana.
Na Mwandishi Wetu



No comments:
Post a Comment