Gazeti la Mbunge Sued Kubebea Hatarini Kufungiwa... Serikali Yalitaka Kujieleza...#share.
GAZETI la Mwanahalisi linalomilikiwa na Mbunge wa Ubungo Sued Kubenea huenda likakumbwa na kadhia ya kufungiwa kwa kuchapisha habari zilizokinyume na misingi ya uandishi wa habari.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, DK. Hassan Abbasi ameutaka uongozi wa gazeti hilo kujieleza kwa nini wasipewe adhabu.
DK. Abbasi amedai kuwa wamekuwa wakiuonya uongozi wa gazeti hilo mara kwa mara kwa uandishi wa habari zinazokiuka misingi ya taaluma hiyo lakini bado wamekuwa wakikiuka.
"Gazeti la mwanahalisi limekuwa likiendelea kuandika habari zinazokiuka misingi ya uandishi wa habari, sharia za nchi na hata zile za kimataifa zinazohusu wajibu wa uhariri kwa taaluma hii,"
"Serikali imekuwa mara kadhaa ikiwakumbusha kwa maandishi wamiliki na wahariri wa gazeti hilo juu ya wajibu wao katika kufuata misingi hiyo, " amesema Abbasi.
Aidha DK. Abbasi hajataja habari yoyote ile inayodaiwa kukiuka misingi ya kitaaluma.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment