GUMZO: Mbunge Nkamia apeleka Mswada wa Uchaguzi kila miaka 7.. 'Nchi kama Rwanda wanafanya Uchaguzi kila baada ya miaka 7 na mambo yao safi..' #share
Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia anatarajiwa kuwasilisha muswada binafsi bungeni akilitaka bunge kufanya marekebisho ya katiba ili kutoa nafasi kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania uwe unafanyika baada ya miaka Saba badala ya mitano ya sasa.
Nkamia amekaririwa akisema kuwa kufanyanuchaguzi kilanbaada ya miaka mitano ni gjarama kubwa kwa nchi masikini kama Tanzania. Amesema katika kipindi cha miaka mitano nchi imekuwa na uchaguzi wa serikali za.mitaa miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu na hivyo kufanya gharama za uchaguzi kuwa kubwa na serikali badala ya kushughulikia kero za wananchi imekuwa ikishughulikia kutafuta fedha za maandalizi na uchaguzi kwa muda mrefu.
Nkamia ambaye anamalizia shahada yake ya pili ya uhusiano wa kimataifa katika chuo kikuu cha Dodoma amesema ameanza hatua za awali.za kuandaa muswada huo ikiwa ni pamoja na kuutarifu uongozi wa chama chake ndani ya bunge na kesho anatarajiwa kumwandikia Spika kuhusu kusudio hilo
"Tanzania ni nchi masikini tunatumia pesa nyingi kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ndani ya kipindi kifupi na hivyo kusababisha fedha nyingi badala ya kushughulikia huduma za jamii kama maji, barabara, zahanati na elimu.. na badala yake tunatumia fedha hizo kwenye uchaguzi" mekaririwa akisema.
Nchi ndogo kama Rwanda inafanya uchaguzi kila baada ya miaka saba na ndio miongoni mwa nchi za Afrika zinazopiga hatua kimaendeleo.
Nkamia amewaomba Watanzania na wadau wote kutafakari kwa kina na kuacha siasa za mihemuko katika kujadili suala hili litakapofikia hatua ya mjadala ili Taifa letu lisonge mbele kimaendeleo

No comments:
Post a Comment