NEWS: TAKUKURU yamtaja mmiliki wa 'vichwa tata vya Treni' bandarini.. yaainisha ukiukwaji wa taratibu za kiutawala wakati wa uagizaji.. #share

TAKUKURU imesema kuwa mmiliki wa vichwa vya Treni vilivyoko Bandarini ni kampuni ya Electro-Motive Diesel lakini hakuna mkataba wa mauziano kati yake na TRL.



Rais aliviagiza vyombo vya usalama kufuatilia sakata la vichwa hivi baada ya ununuzi wake kuwa na utata na Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano kusema haina taarifa za ununuzi wake.

Mkurugenzi wa TAKUKURU amesema katika sakata hili inawezekana taratibu za kiutawala zilikiukwa au makosa ya jinai yalitendwa.

Lakini wao kama TAKUKURU bado wanaendelea kufuatilia kwasababu watuhumiwa wote wameshahojiwa na vielelezo vyote wamevipata.

Kama kuna makosa ya kijinai watapeleka jalada kwa Mwendesha Mashitaka wa Serikali.
Source: JF

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search