Hii Hapa Kauli ya Zitto Kabwe, Baada ya Nyumba Yake Kuteketea Kwa Moto...#share


MBUNGE wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, amethibitisha nyumba yake anayoishi katika eneo la Kibingo, Mji Mdogo wa Mwandiga Kigoma kuteketea kwa moto.


Aidha amesema kutokana na ajali hiyo hakuna mtu aliyeumia na amewashukuru Jeshi la Zima Moto, majirani pamoja na wananchi kwa ujumla kwa ushirikiano waliotoa hadi kuuzima moto huo.

Zitto amebainisha kuwa kwa sasa Jeshi la Polisi linafanyia kazi suala hilo ili kujua chanzo cha ajali hiyo.



"Tumepata ajali kidogo. Nyumba yangu ninayoishi katika eneo la Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga, Kigoma imeteketea kwa moto jioni hii (jana). Alhamdulillah, kuwa hakuna binaadam aliyeumia,".

"Nawashukuru Jeshi la Zimamoto, majirani zangu pamoja na wananchi wenzangu kwa ushirikiano walioutoa mpaka kuuzima moto husika. Kwa sasa Jeshi la Polisi wanafanyia kazi kujua chanzo cha ajali,". ameandika Zitto Kupitia mitandao yake ya kijamii.

Kutokaana na jeshi la polisi kuendelea na uchunguzi juu ya suala hilo, itto amewataka wananchi kuwa watulivu wakati huu polisi wanapoendelea na uchunguzi.



Na Abraham Ntambara

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search