Jeshi la Polisi nchini Latoa Onyo Kwa Wahalifu wa Mtandaoni...#share
JESHI la Polisi nchini limesema limejipanga vyema kupambana
na viotendo vya uhalifu wa mitandaoni huku likibainisha kuwa vitendo hivyo
vimepungua kwa mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Msemaji wa jeshi
hilo Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Barnabas Mwakalukwa,
wakitoa taarifa ya hali ya makosa ya kimtandao yalivyo kwa hivi sasa, amesema
kuundwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao imesaidia kupunguza uhalifu huo.
Akitaja takwimu za makosa hayo kwa mwaka jana amesema uhalifu
wa kupitia ATM, makosa yaliyolipotiwa ni 260 , wizi kwa njia ya simu matukio
3233, lugha ya matusi matukio 911, matukio ya uchochezi 115 kutishia kuua 1210,
vitisho vya kawaida 317.
“Lakini ukilinganisha mwaka huu kuanzia Januari hadi Septemba
matukio ya uhalifu yapo 1663 na ni kwamba lugha ya matusi yako matukio 327,
lakini kutishia kuua ni matukio 304, utapeli 36 na kuna kesi ambazo
zimelipotiwa,” amesema ASP Mwakalukwa.
Akifafanua kuhusu kesi zilizoripotiwa ni kwamba mwaka jana
zulikuwa 573 ukilinganisha na mwaka huu wenye kesi 553. Pia watuhumiwa
waliokamatwa mwaka jana ni 1080 ukilinganisha na watuhumiwa 315 kwa mwaka huu
huku waliopelelezwa na kutiwa hatiani kwa mwaka uliopita walikuwa watu 88 wakati mwaka huu 19.
ASP Mwakalukwa amewataka wananchi wanapokumbwa na uhalifu wa
jinsi hiyo kuripoti kituo cha polisi badala ya kuzungumza na vyambo vya habari
kwani wataharibu uchunguzi wao.
Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Watumiaji na Watoa Huduma za
Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Thadeo Ringo amesema
changamoto kubwa za kihalifu wanazokumbana nazo ni mbili, upotevu wa fedha kwa
njia ya simu na ATM.
Amesema kwa njia ya simu ni kwamba mara nyingi watu wamekuwa
wakikosea namba wanapotuma fedha kwani wamekuwa wakikosea namba na kutuma kwa
mtu ambaye si mlengwa. Kutokana na hali hiyo aliwataka wananchi kabla ya kutuma
fedha kujiridhisha kwanzakama unayetaka kumtumia ndiye.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment