Breaking: Balozi Mahiga 'aitisha press'.. akanusha ya Tanzania kushirikiana na Korea Kaskazini,..#share
SERIKALI imesema haina uhusiano wa karibu na nchi ya Korea Kaskazini huku ikibainisha kuunga mkono juhudi za Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa kupinga utengenezaji na matumizi ya silaha za Nyuklia.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kuwepo taarifa zinazodai Tanzania ina uhusiano wa kibiashara na baadhi ya makampuni kutoka nchi hivyo kwenda kinyume kwa kukiuka vikwazo vilivyowekwa na baraza hilo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga wakati akizungumza na wanahabari kuhusu kuwepo taarifa hizo.
Ameabainisha kuwa taarifa hizo zinaeleza Tanzania ni kati ya nchi 11 zinazoshirikiana na nchi hiyo huku akisisitiza kipindi cha nyuma kulikuwa na ushirikiano katika suala la ununuzi wa vifaa vya ulinzi na usalama na kwamba baada ya tamko kutoka baraza hilo Serikali ilianza kuchukua hatua za kutoshirikiana na nchi hiyo.
'' Madhara ya nyuklia hayaishii pale yanatawanyika dunia nzima mfano anagalia Japan watoto wanazaliwa walemavu hatuna ugomvi na Korea Kaskazini ila kutokana na kitendo chao kutumia silaha hizo tumeondoa mahusiano,'' alisema Dk Mahiga.
Waziri Mahiga amesema nchi haikufanya hivyo kwa kushinikizwa ila takwimu zimeweka wazi silaha hizo ni tishio la amani ya dunia na kwamba kuna mikataba mingi ya kimataifa inapinga matumizi ya nyuklia.
Ameongeza kuwa suala la baadhi ya meli za makampuni ya nchi hiyo kupandisha bendera za Tanzania si za kweli na kuweka wazi kuwa Serikali italifanyia uchunguzi suala hilo na kupeleka taarifa kwenye baraza hilo.
Ameifafanua kuwa ripoti ya baraza hilo inayoeleza bado kuna ushirikiano wa kibiashara katika sekta ya ulinzi imepitwa na wakati, akitilia mkazo kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na mataifa makubwa yaliyomo ndani ya baraza hivyo itatolewa majibu kabla hajaenda kushiriki mkutano wa UN na akiwa huko atafanya mazungumzo na wawakilishi wa nchi hizo.
Pia amesema biashara ilifanyika kabla nchi hiyo haijawekewa vikwazo na baraza hilo na kuwaondoa hofu wananchi kuwaomba waendelee kuwa watulivu kwani Tanzania sehemu ya UN
No comments:
Post a Comment