Katibu Mkuu CUF Maalim Seif Amjulia Hali Tundu Lissu...Soma Habari Kamili na Matukio360
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif leo Septemba 26, 2017 ameingia
jijini Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama Cha Wanasheria
Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi.

Mwenyekiti wa kamati ya muda ya uongozi CUF, Julius Mtatiro
amethibitisha hilo na kusema kuwa kiongozi huyo na baadhi ya viongozi wa CUF
wamewasili nchini Kenya kwa ajili ya kwenda kumuona Tundu Lissu.
"Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif
Hamad ameingia jijini Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais
wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Mhe. Tundu Antipas Lisu (leo) ambaye
amelazwa Hospitali ya Nairobi" alisema Julius Mtatiro
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa
risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na kisha baadaye
kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment