Kauli ya Zitto ni kwamba uamuzi wa Mahakama ya Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi unatoa somo moja tu kwa Tanzania...Pia awapiga kijembe akina Thabo Mbeki......#share

KUFUATIA uamuzi wa Mahakama ya Juu Kufuta kufuta ushindi wa Uhuru Kenyatta kwa kiti cha Urais kutokana na kuwepo kwa ukiukwaji wa sheria katika uchaguzi huo na kuamuru uchaguzi huo kuruduiwa ndani ya siku 60 kumekuwepo na maoni tofauti tofauti juu ya hatua hiyo.
Kwa upande wa Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo Zitto Kabwe amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa hatua hiyo inatoa somo moja Tanzania kuwa inahitaji KATIBA MPYA.
"Uamuzi wa Mahakama ya Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi unatoa somo moja tu kwa Tanzania-KATIBA MPYA Ni lazima lazima lazima," ameandika Zitto.
Aidha ametoa rai kuwa wasiruhusiwe tena waliokuwa waangalizi katika uchaguzi huo wa Kenya, kuangalia uchaguzi mwingine. Waangalizi hao ni pamoja @JohnKerry@ThaboMbeki@TMALIunisa@JDMahama.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment