bREAKING nEWS: Uhuru Kenyatta akubali yaishe.....asema amejipanga kurudi kwa Wakenya kuomba kura...#share

RAIS Uhuru Kenyatta amekubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Kenya kufuta ushindi wake kutokana na Mahakama kubaini kuwepo kwa kasoro katika uchaguzi uliopita katika ngazi ya Urais.

Kauli hiyo imekuja masaa kadhaa baada ya Mahakama hiyo kutengua matokeo, amesema anaheshimu   utawala wa sheria na kusisitiza wakenya kulinda amani ya nchi na kumtaka kila mtu kuwa mheshimu jirani yake licha ya tofauti walizonazo za kidini, kisiasa na kikabila.

“Nachukua nafasi hii pia kumshukuru Mungu, ni yeye alituumba, ni yeye anayemwezesha kila mkenya kutembea hapa na pale kwa amani, ni kitu kizuri kwa Kenya kuheshimu utawala wa sheria,” amesema Kenyatta.

Aidha amebainisha kuwa wapo tayari kurudi tena kwa wananchi kuomba kura zao kwa ajenda za awali walizojinadi nazo ambazo ni paoja na jinsi watakavyoleta maendeleo ya nchi na wananchi wenyewe.

Pia amewataka wapinzani kujipanga katika uchaguzi huo na kueleza kuwa kikundi cha watu wachache hakiwezi kubadili matakwa ya wakenya zaidi ya milioni 40.

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search