Mauzo ya Hisa DSE Yaongezeka..Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
KIWANGO cha mauzo ya
hisa katika Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE) kimeongezeka kutoka shilingi
bilioni 5.4 wiki iliyopita hadi kufikia shilingi bilioni 53.5 mnamo September 22
mwaka huu .
Ofisa Masoko Mwandamizi wa DSE Mary Kinabo akitoa taarifa ya yeliyojiri kwenye soko la hisa kwa wiki iliyoishia Septemba 22/ 2017 mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam (Picha na Abraham Ntambara).
Kuongezeka kwa mauzo ya hisa hizo kumetokana na kuongezeka
kwa ukubwa wa mtaji katika kampuni ya Kenya Airways kwa asilimia 20 pamoja na
uchumi super market kwa asilimia 12.5pamoja benki ya kibiashara ya Kenya kuongezeka
kwa asilimia 9.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
Ofisa Masoko Mwandamizi wa DSE, Mary kinabo amesema
kuwa ukubwa wamtaji wa kampuni zandani umeongezeka kutoka shilingi milioni 27
hadi kufikia shilingi trioni 9.5
‘’Makapuni yaliyo ongoza wiki hii katika mauzo ya hisa
nipamoja na Benki ya biashara ya CRDB ,DCB Pamoja na Soko lahisa la Dar es
salaam’’ amesema kinabo.
Amebainisha kuwa wakati mauzo ya hisa ya kiongezeka kutoka bilioni 5.4 hadi kufikia
shilingi bilioni 53.5 mauzo ya hati fungani hadi kufikia September mwaka huu
yameongezeka kutoka bilioni 22 hadi kufikia bilioni 36.
Aidha amebainisha kuwa mauzo hayo yalitokana na hati fungani kumi nan ne (14) za serikali zenye jumla ya thamani y ash.bilioni 40 kwa jumla ya gharama ya sh.bilioni 36.
Amesema kiashiria cha kampuni
zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 30 kutoka pointi 2,098 hadi pointi 2,128 kutokana na kupanda kwa bei za hisa kwenye kampuni ya Kenya Airways, Uchumi Supermarket Ltd na Kenya Commercial Bank.
Amesema kiashiria cha kampuni
zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 30 kutoka pointi 2,098 hadi pointi 2,128 kutokana na kupanda kwa bei za hisa kwenye kampuni ya Kenya Airways, Uchumi Supermarket Ltd na Kenya Commercial Bank.
Hata hivyo Kinabo amebainisha kuwa kiashiria cha kampuni za
ndani TSI kimepanda kwa pointi 11 kutoka 3.704 hadi pointi 3,715 huku kiashiria
cha sekta ya viwanda (IA) kimepanda kwa pointi 26 kutoka pointi 5052 hadi
pointi 5078.
Ameeleza kwamba kiashiria cha huduma za kibenki na fedha (BI)
wiki hii imepungua kwa pointi 2 kutoka pointi 2,520 hadi pointi 2,518 na
kiashiria cha sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali
kwenye wastani wa pointi 2,475.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment