Sports News: Sakata la Neymar na Cavanni Lachukua Sura Mpya...Ni Baada ya Cavanni Kupuuza Ombi la Mabosi wake wa PSG..Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
KUFUATIA kutoelewana baina ya wachezaji wawili wa klabu ya
PSG Edison Cavanni na Neymar kulikotokana na hali ya kutofautiana kwa
kugombania kupiga peneti kulikotokea hivi karibuni.
Ni kwamba taarifa hizo
zinaendelea kutawala vichwa vya habari, baada ya mvurugano huo ambpo siku
kadhaa zilizopita inasemekana wachezaji hao walipatana baada ya Neyma kuomba
msamaha kwa kitendo hicho.
Hata hivyo kumeibuka jipya, inasemekana mabosi wa klabu ya
PSG walikaa chini na Edison Cavanni na kumuomba amruhusu Neymar kupiga penati
huku pia wakitaka kumpa kiasi cha pesa ili kukubali.
PSG walitaka kumpa Cavanni kiasi cha €1million ambayo ni pesa ambayo wangempa Cavanni mwisho wa msimu kama akimalizia mfungaji bora lakini sasa wakataka kumpa kiasi hicho ili amuachie Neymar kupiga tuta.
Edison Cavanni amekataa kiasi hicho cha pesa na hii inamaanisha kwamba hayuko tayari kumuachia mtu mwingine apige penati na anaona ni bora akose kiasi hicho cha pesa kuliko kuacha kupiga penati.

Inadaiwa kwamba baada ya Neymar na Cavanni kugombana ilimbidi
tajiri wa PSG Nasser El Khaifi kukaa na Cavanni ili kujaribu kumshawishi kuhusu
kumpa Neymar penati lakini Cavanni amekataa.
Mbaya zaidi inadaiwa kwa sasa kumeanza kuwa na makundi katika
klabu hiyo kwani kuna kundi kubwa ndani ya PSG linalomsuport Cavanni huku
kikundi kingine kidogo kinachoundwa na Wabrazil pekea yao wakiwa wanamuunga
Neymar.
Hali hii inamuweka njia panda kocha wa klabu hiyo Unai Emery
kwani ni wazi na yeye anataka Cavanni aendelee kupiga penati katika timu hiyo
lakini tajiri wa timu anaonekana anataka Neymar awe kila kitu.
No comments:
Post a Comment