Kubenea adai Tundu Lissu anawajua waliompiga risasi.. #share
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea ameeleza kuwa Tundu Lissu amesema kwamba anawajua waliompiga risasi na kama Jeshi la Polisi litawakamata anaweza kuwatambua kwa sura.
Aidha, Kubenea amedai kuwa Tundu Lissu amesema washambuliaji hao walianza kumfuatilia kuanzia Tegeta-Dar na baada ya kugundua anafuatiliwa aliweza kuwakimbia hadi Dodoma na kuwaacha.
Kubenea ameyasema maneno hayo mapema leo alipopewa nafasi ya Kusalimia katika ibada iliyofanyika kwenye kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo jijini Dar Es Salaam.
Na Mwandishi Wetu



No comments:
Post a Comment