Lema Amjibu Waziri Ummy...Ni Kuhusu Kauli yake Kuwa Serikali Iko Tayari Kugharamia Matibabu ya Lissu...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360...#share
MBUNGE wa Arusha Mjini Gobless Lema amemjibu Waziri wa Afya,
Ummy Mwalimu kuhusu kauli aliyotoa jana kuwa serikali ipo tayari kumtibu Mwanasheria
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika (TLS) Tundu Lissu kama familia yake itapeleka maombi maalumu kwa serikali.
Akimjibu juu ya suala hilo Lema amesema kuwa familia ya Lissu
haijashindwa kumgharamia matibabu.
Lema amesema anaamini familia ya Tundu Lissu ni Watanzania
wote ambao wanapenda haki na Demokrasia ndani ya nchi, na wote ambao wanaumizwa
na jambo hilo bila kujali itikadi zao hivyo watachanga shilingi moja moja kwa
ajili ya matibabu ya Tundu Lissu na hata ikibidi mali zao watauza ili kuweza
kumuwezesha Tundu Lissu kupata matibabu.
"Familia ya Lissu ni Watanzania wote wanaopenda utawala
wa sheria, Utawala wa Demokrasia, familia ya Lissu ni Watanzania wote bila
kujali itikadi zao ambao wanajisikia vibaya kwa matendo ya kihalifu kwa wabunge
kupigwa risasi hadharani na bunge lisichukue hatua stahiki hii ndiyo familia ya
Lissu, mtu yoyote ambaye anaguswa na ubinadamu na familia hii haijashindwa
kumlipia matibabu tutachanga shilingi moja moja ikiwa ni lazima sana tutauza
hata mali zetu kuhakikisha kwamba Mhe. Tundu Lissu akosi fedha za
matibabu" amesema Lema
No comments:
Post a Comment