Mwenyekiti Chadema Mbowe Aivaa Serikali Kuhusu Kumtibu Lissu...Habari Kamili na Matukio360...#share


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amezungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari  kwa mara ya kwanza baada ya kurudi Dar es Salaam kutoka Nairobi anakopatiwa matibabu Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi September 7, 2017 jijini Dodoma na watu wasiojulikana. 

Mbowe ameeleza hali ya Lissu.
"Shambulio lile halikuwa kwa Lissu peke yake, lilikuwa shambulio la Chama, kauli ya Haki, Ubinadamu na Watanzania kupitia Lisu." Mbowe.

"Lissu amebeba majeraha mengi, maumivu makali kwa kauli zake za kulitetea Taifa lake, kuwatetea Watanzania wenzake na kudai haki." Mbowe.

"Nianze na habari njema; Tundu Lissu anawasalimu sana. Nimeachana naye Nairobi jana mchana nikamwambia nitazungumza na Watanzania." Mbowe.

"Akaniomba nimpelekee salamu zake kwamba Mungu anaendelea kumpigania na In Shaa Allah baada ya muda atarejea kwa mapenzi yake." Mbowe.

"Tundu Lissu yupo chini ya ulinzi mkali sana saa 24 nje na ndani... hatuwezi kufanya uzembe tena" - Mbowe.

"Mashine yetu 'Lissu' itarudi barabarani salama kabisa ikiwa timamu, nataka niwaeleze ufahamu wake uko vizuri 100%" 
"Lissu hakukata kauli mpaka anaingia theatre, pamoja na majeraha yote hajawahi kukata kauli" - Mbowe.

"Hali ya mgonjwa, Lissu alifikishwa Nairobi usiku saa sana, hali yake ilikuwa ngumu sana. Madaktari walitupokea na kuanza kumhudumia." Mbowe

"Madaktari wanasema ni miujiza kutoka salama bila kukatwakatwa kwa risasi ktk shambulio kama la Lissu" Mbowe.

"Lissu anatibiwa na kundi kubwa la madaktari na ningependa niwatambue waingie kwenye rekodi kwa kazi ya ziada kuokoa maisha ya Lissu." Mbowe

"Kabla ya madaktari wa Nairobi, niwashukuru madaktari wa Hospitali ya Dodoma. Kama wasingefanya wajibu wao wa msingi tusingesafiri na Lissu"

"Kazi kubwa iliyofanywa na madaktari wa dodoma tusiipuuze, ilituwezesha kufika Nairobi akiwa hai. Ilikuwa ni miujiza kila mmoja alishangaa."

"Ikasemwa Ndege ya Lissu imelipiwa na wanaCCM, hata ingelipiwa na CCM bado si shida ila ukweli imelipiwa na Chadema" Mbowe.

"Kuna presha ya kumpeleka nchi tofauti sita; wapo waliotaka apelekwe A. Kusini, wengine India, Ubelgiji, Ujerumani, UK na USA" Mbowe

"Kama kiongozi wa Chama nadiriki kusema kwamba mshukiwa namba moja wa shambulio la Lissu ni vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi hii" Mbowe.

"Hilo nalisema bila kumung'unya maneno, viashiria vyote vya tukio lile tangu linatokea kauli na kusita kwa viongozi na kauli za kujiosha."

"Ni nani katika vyombo vya ulinzi na usalama, simjui lakini ni vigumu sana kusema tukio la ujambazi, hakuna ujambazi pale." Mbowe.

"Watu wetu wamepotea, watu wetu wameuawa, wanapigwa risasi mchana kweupe na hakuna hatua ya maana inayofanyika." Mbowe.

"Michango ya TZ ni mil.52, mil.43 zilizochangwa Bungeni bado hatujapewa, wa Marekani wamemchangia Lissu USD 20000" 

"Nimalizie kwa gharama za matibabu. Hakuna kificho kila kitu kimewekwa humu. Mpaka juzi gharama zilifikia Ksh Milioni 6.7." Mbowe.

"Ksh Milioni 7.4 ni sawa na Tsh Milioni 162.8 kwa wiki mbili za matibabu lakini tunasema hata zingekuwa Bilioni, zimemuokoa Lissu." Mbowe.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search