Mahakamani Kisutu: Mholanzi Adai Kuchaniwa Pasport Yake na Polisi...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
RAIA wa Uholanzi Monique Amanzi mwenye (28) ameieleza
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Septemba 22, 2017 kuwa alichaniwa Passport
yake na Ofisa wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani (Trafiki).

Mholanzi huyo anakabiliwa na tuhuma za kuishi nchini bila
kibali.
Amanzi ambaye pia anahusishwa na biashara ya kujiuza,
alisomewa kosa lake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa na Wakili wa
Uhamiaji Novatus Mlay ambapo Wakili huyo alidai kuwa September 11, 2017 Idara
ya Uhamiaji Makao Makuu, Kurasini Temeke ilimbaini kuwa anaisha nchini kinyume
na sheria.
Baada ya kusomewa Amanzi alikana kosa, ambapo alidai kuwa
rafiki yake wa kiume ambaye ni Polisi Kitengo cha Usalama wa Barabarani
anayefanya kazi maeneo ya Victoria Makumbusho alichana hati yake ya kusafiria
akidai baada ya kuchanwa kwa hati hiyo aliripoti Polisi Kinondoni miaka
miwili iliyopita lakini alipoteza RB na kwamba ana watoto watatu ambapo mmoja
amefariki.
Miongoni mwa watoto hao wawili ni wa mume wake Ibrahimu Abas ambaye
alikuja nae hapa nchi lakini walitengana na kumpata Trafiki ambaye alizaa naye
mtoto mmoja bahati mbaya akafariki.
Alidai kuwa aliwahi kwenda Uhamiaji lakini hakupata
mafanikio.
Dhamana ya mshtakiwa iko wazi ambapo anatakiwa kuwa na
wadhamini wawili raia wa Tanzania ambao kila mmoja atasaini bondi ya Tsh Milion
Moja ambapo hata hivyo, upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na Hakimu Nongwa
aliahirisha kesi hadi Septemba 27, 2017 kwa ajili ya kutajwa.
No comments:
Post a Comment