Rais Donald Trump Azidi Kuichokonoa Korea Kaskazini.. Kim Jong-un Amjibu...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
RAIS wa Marekani Donald Trump amesaini sheria mpya ya
kuongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini kutokana na mpango wake wa nyuklia,
Trump pia amesema kuwa benki kuu nchini China imeagiza benki nyingine za China
kuacha kufanya biashara na Korea Kaskazini.
Tayari waziri wa fedha wa Marekani ameidhinisha vikwazo hivyo
dhidi ya makampuni ya fedha yanayofanya biashara zake ndani ya Korea Kaskazini.
Hatua hii inakuja katika kipindi cha chini ya wiki mbili
baada ya umoja wa mataifa kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya taifa hilo
kwasababu ya jaribilo lake la hivi karibuni la nyuklia.
Wakati hayo yakiendelea rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
amemuita Tramp mropokaji asiyefikiria na kwamba kauli anazotoa Trump zinamfanya
ajione yuko sahihi kuendelea na mipango yake ya nyuklia.
Katika taarifa isiyo ya kawaida kupitia vyombo vya habari vya
serikali kiongozi wa Korea Kaskazini alisema Trump atajutia hotuba yake ya hivi
karibuni aliyoiotoa kwa Umoja wa Mataifa.
Hali ya wasi wasi imetanda katika kipindi cha wiki za hivi
karibuni kutokana na hatua ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya
masafa marefu, licha ya shinikizo kutoka kwa mataifa tajiri zaidi duniani
kuitaka iachane na majaribio hayo.
No comments:
Post a Comment